December 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mabilioni ya dola yaahidiwa Pakistan

Dola za Marekani

Spread the love

 

MKUU wa misaada ya kimataifa, Martin Griffiths ameahidi kutoa dola bilioni 1.2 kuwasaidia mzozo unaoendelea nchini Pakistani. Anaripoti Helena Mkonyi TUDARCo … (endelea).

Griffiths amesema, mabilioni hayo ya fedha yameahidiwa kutolewa kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Pakistani kutatua mizozo mbalimbali na matatizo yanayowakumba.

Ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa ngazi ya juu mjini Geneva.

Martin ametoa wito kwa wafadhili wote waliopo katika shirika la misaada la kimataifa kutekeleza ahadi zao haraka iwezekanavyo ili kutatua matatizo ya Waafganistani ikiwemo wanawake ambao ndio wanaongozwa kwa kunyonywa na kuonewa nchini humo.

“Jukumu la wanawake na wasichana ni muhimu mno kama sehemu yoyote ile, wanastahili kupata elimu, wanastahili kupata haki zao muhimu kama watu wengine na huduma zingine muhimu kama ilivyo kwingineko duniani,” alisema Griffiths.

error: Content is protected !!