September 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kinachoendelea kesi ya kina Mbowe, RPC Kingai anatoa ushahidi

Spread the love

 

KESI ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili kiongozi wa chaa kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, inaanza kusikilizwa mfululizo kuanzia leo Jumatano, tarehe 15 Septemba 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea). 

Mbali na Mbowe wengine; ni Halfani Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Lingwenya.

Jaji anayesikiliza kesi hiyo Mustapha Siyai ameingia ndani ya chumba cha Mahakama na kuiita kesi hiyo.

Wakili wa serikali mwandamizi, Robert Kidando, ameieleza Mahakama kuwa wamekuja mahakamani kusikiliza shauri na wamewaleta mashahidi wawili.

Miongoni mwa mashahidi waliopo tayari mahakamani kutoa ushahidi ni, Kamanda wa Polisi wa Kinondoni (RPC), Ramadhan Kingai.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

error: Content is protected !!