Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Michezo Kikwete: Yanga itaipiga Simba
MichezoTangulizi

Kikwete: Yanga itaipiga Simba

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete
Spread the love

 

JAKAYA Mrisho Kikwete, Rais mstaafu wa Tanzania amesema, atafurahia iwapo Yanga itaibuka na ushindi dhidi ya mtani wake, Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jumapili, tarehe 27 Juni 2021, katika mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika ukumbi wa DYCC-Temeke, mkoani Dar es Salaam.

Yanga na Simba, zitacheza mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara, tarehe 3 Julai 2021, saa 11 jioni, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

 

Kikwete ambaye ni shabiki wa mabingwa hao wa kihistoria amesema “Yanga naipenda, inapofanya vizuri nafurahi sana na inapofanya vibaya nasononeka na matumaini yangu Jumamosi ijayo itafanya vizuri.”

Pia, watani hao wa jadi, watakutana tarehe 25 Julai 2021, katika Uwanja wa Tanganyika, mkoani Kigoma kwenye fainali ya Kombe la Azam Sports Federetion Cup (ASFC).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

error: Content is protected !!