Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Makocha, wachezaji: Kikwete awataka Yanga kuvuta subra
Michezo

Makocha, wachezaji: Kikwete awataka Yanga kuvuta subra

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete
Spread the love

 

RAIS mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ameutaka uongozi na wanachama wa mabingwa wa soka nchini humo, Yanga kuwa wavumilivu kufikia mafanikio pindi wanaposajili wachezaji na makocha. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha na wachezaji, hayawezi kuwa na tija na kuleta mafanikio kwani kunakuwa hakuna muunganiko.

Tangu kuanza kwa msimu wa ligi kuu Tanzania Bara 2020/21, Yanga imekuwa na makocha wanne huku ikibadili robo tatu ya kikosi kilichoshiriki ligi ya 2019/20.

Kikwete amesema hayo leo Jumapili, tarehe 27 Juni 2021, wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa Yanga, uliofanyikia ukumbi wa DYCC-Temeke, mkoani Dar es Salaam.

Mkutano huo, ilikuwa na lengo la kufanya mabadiliko ya katiba ya klabu hiyo kongwe nchini, ili kuiwezesha kuendeshwa kisasa.

Mukoko Tonombe mchezaji wa klabu ya Yanga

“Muwe makini katika kutafuta kocha, wachezaji ili msilazimike kufanya mabadiliko ya mara kwa mara. Kufanya mabadiliko ya mara kwa mara yana sura mbili, ama mliyemchukua hakuwa makini kama anaweza kufundisha au kucheza, au uzembe au iko namna,” amesema Kikwete, aliyekuwa Rais wa Tanzania kati yam waka 2005 hadi 2015.

Huku akishangiliwa na wanachama amesema “maana inaweza kuweko namna na ikawa mambo magumu sana. Hili mliangalie.”

“Wakati mwingine wanachama tunapaswa kuwa na subra, mtu hawezi kuja leo, mabadiliko yakaja mechi inayofuata.”

“Wachezaji hawawezi kuja leo mnataka ubingwa, yaani kocha anakuja leo, katikati ya msimu mwingine, mwisho wa msimu mwingine halafu mnataka mabadikiko,” amehoji.

Nasriddine Nabi, Kocha wa Yanga (katikati)

Kikwete amesema, suala hilo hilo linapaswa kuangaliwa kwa maini kwani “kila mnaposikia kuna mchezaji mzuri mnamleta, hawajazoena lazima mliangalie hili.”

Pia, amewataka kuzingatia maslahi ya makocha na wachezaji.

“Hakikisheni makocha na wachezaji wanahudumiwa vizuri, wasiwe wanadai mishahara ya mechi mbili au tatu halafu ukiwapeleka kwenye mechi ngumu wakashindwa unasema wamekuhujumu, sasa wamekuhujumu vipi hujamlipa mishahara?”

“Msipofanya hayo, mtageuka kuwa wategemezi wa kamati za ufundi badala ya kuwa wategemezi wa benchi la ufundi. Kuna benchi la ufundi ndiyo rasmi na mkiyaendekeza ya kamati za ufundi hamuwezi kusonga mbele,” amesema

Amesema, mafanikio yapo kwenye kuwekeza kwa wachezaji na makocha wazuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!