Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bil 3.61 kutumika ujenzi barabara ya Lumecha – Londo
Habari Mchanganyiko

Bil 3.61 kutumika ujenzi barabara ya Lumecha – Londo

Spread the love

 

SERIKALI imetenga jumla ya Sh. 3.61 bilion kwa ajili ya matengenezo ya barabara ya Lumecha – Londo. Anaripoti Jemima Samwel DMC…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Godfley Msomgwe, Naibu Waziri wa Ujenzi leo Jumatatu tarehe 10 Mei 2021, katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, jijini Dodoma akijibu swali la Jacqline Msongozi, Mbunge wa Viti Maalumu.

 “Je, ni lini serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Lumecha – Londo – Kilosa kwa Mpepo, inayounganisha Mkoa wa Ruvuma na Morogoro kwa kiwango cha lami?” amehoji Msongozi.

Waziri Msongwe amesema, barabara hiyo ni sehemu ya barabara kuu ya Mikumi – Kidatu – Ifakara – Lupiro/Mahenge – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Lumecha yenye jumla ya kilometa 512, ambayo inaunganisha Mikoa ya Ruvuma na Morogoro.

“Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii, ulikamilika mwaka 2018 ikiwa ni lengo la serikali kujenga barabara yote kwa kiwango cha lami.

“Hadi sasa, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mikumi– Kidatu (km 35.2) na ujenzi wa Daraja la Magufuli (m 384) pamoja na barabara unganishi (km 9.142), umekamilika. Ujenzi wa sehemu ya Kidatu – Ifakara (km66.9) unaendelea na umefikia asilimia 22.6,” Waziri Msongwe amesema.

Amesema, kwa upande wa barabara hiyo kuanzia Lupiro/Mahenge – Malinyi– Kilosa kwa Mpepo – Londo – Lumecha, serikali inaendelea kutafuta fedha za kuanzaujenzi kwa kiwango cha lami ikiwemo sehemu ya Lumecha – Londo – Kilosa kwa Mpepo.

“Wakati juhudi za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami zikiendelea, serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Ruvuma na Morogoro itaendelea kuifanyia matengenezo barabara hii kutoka Ifakara – Lupiro/Mahenge – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Lumechakila mwaka ili iweze kupitika majira yote ya mwaka.

“Katika mwaka wa fedha 2020/21, barabara hii imetengewa jumla ya Sh.361.51 Milioni kwa ajili ya matengenezo mbalimbali. Kati ya fedha hizo, Sh. 985.58 milioni ni kwa ajiliya sehemu ya barabara ya Lumecha – Londo ambayo iko mkoa wa Ruvuma,” amesema Msongwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!