Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaibwaga CCM, ACT-Wazalendo
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yaibwaga CCM, ACT-Wazalendo

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeshinda Tuzo ya Watu, Taasisi na Chapa, zinazoongoza mtandaoni (Tanzania Digital Awards), kwenye kipengele cha chama bora cha siasa  mtandaoni (Best Political Party Use of Social Media). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Chadema kimetwaa tuzo hiyo baada ya kupata kira nyingi katika kipengele hicho cha  chama bora cha siasa, katika kutumia teknolojia ya kidigitali kuchochea maendeleo.

Chama hicho kimevibwaga vyama vitatu vilivyokua vinachuana katika  kundi F, kwenye kipengele cha uongozi bora katika teknolojia ya kidigitali.

Tuzo hiyo ilitangazwa jana tarehe 25 Desemba 2020.

 

Vyama vilivyokuwa vinasaka tuzo hiyo ni, ACT-Wazalendo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa

Tuzo hiyo imetolewa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mwaka huu.

Katika tuzo hiyo, wananchi walipiga kura kuchagua chama cha siasa bora katika kutumia mitandao ya kijamii kuongoza wananchi kwenye kuleta maendeleo.

Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango wa watu na taasisi ambazo zinatumia kifanisi na kwa ubunifu majukwaa na teknolojia za kidigitali kuhamasisha na kuchagiza maendeleo ya kudumu katika mitandao na jamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Wanaotaka kujifunza ZEC kwao kukoje?

Spread the loveMKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Biteko, Nape wanadanganya?

Spread the loveKWA mila na desturi zetu za Kiafrika mkubwa huwa hakosei,...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miamka 60 ya Muungano: Tunakwama wapi?

Spread the loveRAIS wa Jamhuri, Samia Suluhu Hasssan, Ijumaa iliyopita, aliongoza mamilioni...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

error: Content is protected !!