CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeshinda Tuzo ya Watu, Taasisi na Chapa, zinazoongoza mtandaoni (Tanzania Digital Awards), kwenye kipengele cha chama bora cha siasa mtandaoni (Best Political Party Use of Social Media). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Chadema kimetwaa tuzo hiyo baada ya kupata kira nyingi katika kipengele hicho cha chama bora cha siasa, katika kutumia teknolojia ya kidigitali kuchochea maendeleo.
Chama hicho kimevibwaga vyama vitatu vilivyokua vinachuana katika kundi F, kwenye kipengele cha uongozi bora katika teknolojia ya kidigitali.
Tuzo hiyo ilitangazwa jana tarehe 25 Desemba 2020.
Vyama vilivyokuwa vinasaka tuzo hiyo ni, ACT-Wazalendo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
Tuzo hiyo imetolewa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mwaka huu.
Katika tuzo hiyo, wananchi walipiga kura kuchagua chama cha siasa bora katika kutumia mitandao ya kijamii kuongoza wananchi kwenye kuleta maendeleo.
Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango wa watu na taasisi ambazo zinatumia kifanisi na kwa ubunifu majukwaa na teknolojia za kidigitali kuhamasisha na kuchagiza maendeleo ya kudumu katika mitandao na jamii.
Leave a comment