Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kenya kufungua shule Januari 2021
Kimataifa

Kenya kufungua shule Januari 2021

Spread the love

SERIKALI ya Kenya imesema, shule za msingi na sekondori nchini humo zitafunguliwa Januari 2020. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu,Profesa George Magoha alipozungumza na waandishi wa habari leo Jumanne tarehe 7 Julai 2020.

Profesa Magoha alikuwa anatoa taarifa ya kufunguliwa shule baada ya kufungwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita kutokana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19).

Hadi jana Jumatatu tarehe 6 Julai 2020, maambukizo yalikuwa 8,067, waliopona 2,414 na waliopoteza maisha wakiwa 164 huku idadi ya waliopomwa corona wakiwa 191,394.

Waziri huyo amesema, mitihani ya taifa kwa shule za msingi na sekondari haitafanyika mwaka 2020 na itasubiri zitakapofunguliwa mwaka 2021. 

Profesa Magoha amesema,walipanga wanafunzi wa darasa la nane na  kidato cha nne warudi shuleni ili kufanya mitihani ya taifa mwaka 2020 imeshindikana kutokana na corona kuendelea kuwepo.

Amesema, uamuzi huo wameuchukua baada ya majadiliano baina ya Serikali na wadau wa sekta ya elimu kuangazia suala hilo la kufunguliwa au kutokufunguliwa.

Profesa Magoha amesema, shule zitafunguliwa ikiwa idadi ya maambukizo ya corona yatapungua kwa siku 14 mfululizo.  

Kuhusu vikuu,Profesa Magoha amesema, vitafunguliwa kwa awamu huku wasimamizi wakitakiwa kutekeleza mwongozo uliokwisha kutolewa na wizara ya afya nchini humo na watakaokaidi vyuo vyao vitafungwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!