Saturday , 4 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mauaji ya watu 59 Nigeria
Kimataifa

Mauaji ya watu 59 Nigeria

Spread the love

WATU 59 wameuawa katika shambulio lililofanywa na waasi kwenye Kijiji cha Borno, kilichopo Kaskazini mwa Nigeria jana jioni tarehe 9 Juni 2020Chombo cha habari cha Reuters kimeeleza…(endelea).

Waasi hao walivamia kijiji hicho na kuteka watu huku wakipiga risasi wengine pamoja na kupora mali za raia hao. Hata hivyo, mpaka sasa hakuna kundi lolote lililoeleza kufanya tukio hilo.

“Ni siku mbaya sana kwetu kushuhudia mauaji haya,” ofisa mwokoaji Kachallah Bumu alikiambia kituo hicho. Amesema, wapiganaji hao pia waliiba mifugo.

Pia mji wa Gubio uliopo kimomita 80 kutoka mji wa Maiduguri, umeripotiwa kushambuliwa na waasi. Mamlaka ya Nigeria imetuma kikosi cha polisi 100 kusaka watu hao.

Serikali ya Rais Muhammadu Buhari inalalamikiwa na jamii za kimataifa kwa kushindwa kukabiliana na waasi nchini humo, licha ya kuahidi kukabiliana nao kwenye kampeni zake za uchaguzi mwaka 2015.

Katika miezi ya karibu, kumekuwepo na ongezeko la mauaji nchini humo ambapo zaidi ya watu 36,000 wameripotiwa kuuawa, zaidi ya watu milioni mbili wakilazimika kukimbia maeneo yao Kaskazini mwa nchi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!