SERIKALI ya Tanzania imetoa mwenendo juu ya hali ya maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (Covid-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, alisema mikoa takribani 15, haina wagonjwa wapya wa corona.
Waziri Ummy alitoa taarifa hiyo jana Jumanne tarehe 9 Juni 2020, alipotembelea Kituo cha Afya cha Mkonze, kilichotengwa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa Covid-19, mkoani Dodoma.
Wakati huo huo, Waziri Ummy alisema, mikoa iliyosalia wagonjwa wake wanaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.
Kuhusu kituo cha Mkoze, Waziri Ummy alisema, hakina wagonjwa wa Covid-19, kwa zaidi ya muda wa wiki moja.
“Leo (jana) nimetembelea Kituo cha Mkoze ambacho kilitengwa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa Covid-19 mkoani Dodoma.”
“Nina furaha kuwataarifu kwamba, hakuna mgonjwa mpya kwa zaidi ya wiki. Hadi kufikia leo (jana), Dodoma na mikoa mingine 15 , haina wagonjwa wa Covid-19,” alisema Waziri Ummy.
Hata hivyo, Waziri Ummy hakuitaja kwa majina mikoa hiyo 15.
Leave a comment