Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI
AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha Sh. 980 bilioni na Serikali ya Marekani, kwa ajili kuongeza nguvu katika mapambano ya kudhibiti Virusi vya Ukimwi (VVU) na Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yalibainishwa jana Jumatatu na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, jijini Dar es Salaam, katika kikao cha kupitisha bajeti ya Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR), katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.

“Tunaishukuru sana Serikali ya Marekani kwa kuendelea kuipatia Tanzania msaada kwa zaidi ya miaka 20 kwa ajili ya kupambana na VVU na UKIMWI, ambapo kwa sasa watatusaidia Bilioni 980 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo,” alisema Ummy.

Ummy alisema fedha hizo zitasaidia katika utekelezaji wa mikakati ya kuyafikia makundi ambayo bado yana maambukizi mapya kwa kiwango kikubwa kama vile wasichana rika la balehe, wanawake vijana na vijana rika balehe na wanaume vijana.

Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Michael Battle ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kufanya vizuri katika kufikia malengo katika kudhibiti maambukizi mapya na kutoa huduma za kufubaza virusi hivyo kwa waathirika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA wawanoa mama lishe 50 kukabiliana na majanga ya moto

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

error: Content is protected !!