Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ubomoaji Msimbazi Bondeni kuanza Aprili 12, bilioni 52 zalipwa
Habari Mchanganyiko

Ubomoaji Msimbazi Bondeni kuanza Aprili 12, bilioni 52 zalipwa

Spread the love

Zoezi la ubomoaji wa nyumba zilizofidiwa na Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Msimbazi linatarajiwa kuanza rasmi tarehe 12 Aprili 2024, na litawahusu waathirika 2,155 ambao tayari wamelipwa fidia. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hadi kufikia tarehe 21 Machi mwaka huu, waathirika 2,151 kati ya 2,329 tayari wamelipwa kiasi cha Sh bilioni 52.6 kwa mujibu wa orodha ya daftari la kwanza la ulipaji fidia.

Mhandisi Humphrey Kanyenye

Hayo yamesemwa jana tarehe 25 Machi 2024 na Mhandisi Humphrey Kanyenye, Mratibu wa Miradi ya Ushirikiano na Benki ya Dunia TARURA alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za mradi zilizopo Millenium Tower-Kijitonyama, Dar es Salaam.

Mhandisi Kanyenye alieleza kuwa kwa mujibu wa makubaliano ya utekelezaji wa zoezi hilo, waathirika wa mradi ambao wameshakwishapokea malipo yao wanatakiwa kuhamisha mali zao na kupisha eneo la mradi ndani ya wiki sita baada ya kupokea fedha hizo kwenye akaunti zao.

“Waathrika wote wa mradi huu wanafahamu kuwa tuliwapa muda wa kuhama kwa makubaliano maalumu ya kimkataba yaliyowataka kuhama ndani ya wiki sita mara baada ya fedha kuingia katika akaunti zao, muda huo sasa umepita hivyo wanatakiwa kuondoka ili kupisha utekelezaji wa mradi,” alisema Mhandisi Kanyenye.

Alieleza pia kuwa walichelewa kuanza zoezi hilo kwa ajili ya kuwapa muda waathirika wa mradi kubomoa wenyewe kwa hiari ili kuokoa baadhi ya mali zao.

“Lakini pia kuna wale ambao hawakufikiwa katika uthamini wa awali kwa baadhi yao kugomea ama kutoonekana katika maeneo yao, idadi yao ni 466, hawa wameingizwa katika orodha ya daftari la pili ambalo limeshakamilika na litawasilishwa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kusainiwa siku ya jumanne tarehe 26 Machi 2024 tayari kwa kulipwa fidia,” alisema Mhandisi Kanyeye.

Mradi unatekelezwa kwa muda wa miaka sita (2022-2028) kwa gharama takribani Sh 663 bilioni na lengo kuu la mradi ni kuimarisha ustahimilivu kwa kuweka mikakati ya kukabiliana na mafuriko na kuwa na matumizi bora ya ardhi katika eneo la chini la bonde la mto msimbazi ikiwa ni pamoja na kurudisha uoto wa asili katika uwanda wa juu wa bonde la mto msimbazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!