Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kilichomkera JPM kwa Makamba hiki hapa
Habari za SiasaTangulizi

Kilichomkera JPM kwa Makamba hiki hapa

Spread the love

MIONGONI mwa sababu za January Makamba, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kung’olewa kwenye nafasi hiyo, zimetajwa. Anaandika Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza kwenye hafla ya kuwaapisha George Simbachawene (Mazingira) na Hussein Bashe (Kilimo), leo tarehe 22 Julai 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais John Magufuli ameeleza kukerwa na ucheleweshwaji katika kutekeleza maagizo pamoja na fedha za wafadhili kutoonekana kulisaidia taifa kwenye mazingira.

Bila kumtaja jina (Makamba) aliyekuwa akiongoza Wizara ya Mazingira, ameeleza kumekuwepo na fedha nyingi zikitolewa na wafadhili kwa ajili ya mazingira, lakini hazionekani katika utekelezaji wake.

Rais Magufuli alimwondoa Makamba kwenye serikali anayoiongoza jana tarehe 21 Julai 2019, na kumteua Simbachawene kushika nafasi yake huku Hussein Bashe, Mbunge wa Nzega akiteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Akizungumzia kauli ya Simbachawene kuhusu matumizi yasiyoridhisha ya fedha za wafadhili, Rais Magufuli amesema kuwa fedha nyingi zinatolewa lakini hazionekani matumizi yake.

“Fedha nyingi tu zinatolewa na wafadhili lakini haziwi reflected (hazionekani) kwenye miradi husika, kuna miradi mingine ilikuwa hewa kule Rufiji, ikapandwe mikoko mikoko haipo, nataka haya ukayashughulikie.

“Nakumbuka kwenye suala la mifuko ya plastiki, lilichukua muda mrefu… (kama) miaka minne, nikasaini halikutekelezwa. Makamu wa rais akazungumza wee, halikutekelezwa.

“Waziri Mkuu akaenda kulizungumza bungeni, halikutekelezwa mpaka mwishoni nilipotoa amri ya lazima ndipo likaanza kutekelezwa, usiende kufanya hivyo, wewe ukayatekeleze hayo sababu ndiyo uliyoyaapa,” amesema Rais Magufuli.

Kabla ya Rais Magufuli, Simbachawene aliseme kumekuwepo na fedha nyingi zinazoingizwa kupitia taasisi binafsi (NGO), lakini hazionekani kusaidia mazingira.

“Nafahamu kwamba nchi yetu inayo matatizo makubwa sana eneo la mazingira, ziko rasilimali fedha nyingi zinaingia kupitia sekta binafsi-NGOs, hata huduma haziendi moja kwa moja kutatua mazingira bali yanatumika katika utawala zaidi.

“Kinachokwenda kwenye mazingira ni kidogo, hasa tunavyoona hali ya uharibifu wa mazingira kwenye maeneo tunayoishi…,fedha zinazotajwa kuingia katika nchi ni nyingi lakini haziingi kwenye matatizo yaliyiopo,” alisema Simbachawene.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

error: Content is protected !!