April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli ataja sababu kumteua Bashe

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli ametaja sababu za kumteua Hussein Bashe, Mbunge wa Nzega kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Kilimo. Anaandika Regina Mkonde…(endelea).

Akizunguza baada ya kuwaapisha Bashe na George Simbachawene, Rais magufuli leo tarehe 22 Julai 2019, amesema amekuwa akimsikiliza Bashe anapochambua masuala ya kilimo bungeni.

Kutokana na hali hiyo, ameamua kumteua kwenye nafasi hiyo ili yale aliyokuwa akiyazungumza bungeni kuhusu kilimo, akayafanyie kazi.

“Nimekuwa nikikusikiliza vizuri bungeni, umetoa uchambuzi kuhusu kilimo nimeupenda, sasa zile zilikuwa bungeni nataka sasa ukaziweke kwenye practical (vitendo).

“…ni matumaini yangu kwamba yale ambayo uliyafikiria, umeyashauri, ukayatekeleze na mimi ni matumaini sababu sekta ya kilimo ni muhimu,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema, kuna wizi mkubwa kwenye sekta ya kilimo na kwamba anafahamu changamoto inayopata bodi ya sukari.

“Bodi ya sukari inapitia changamoto nyingi sana, inapigwa vita na wafanyabaishara wa sukari, tukasema hapana, haiwezi tunakuwa tunaletewa masukari ya hovyo, yameexpire (yameisha muda wake), yanaletwa kwenye nchi yetu.

“Ni matumaini yangu hayo mkayajoin (mkayaunganishe) vizuri, changamoto zipo, mkisimama kwa umoja wenu mtayamaliza. Kule Kagera tumewaambia wauze kahawa wawekezaji wa nje waje lakini lazima wanunue 1500 na kuendelea kwa kilo,” amesema.

error: Content is protected !!