Spread the love

HAJI Abdallah Khatib, Mhandisi msaidizi wa meli ya MV Mapinduzi, amefariki dunia kwa kujinyonga ndani ya meli hiyo. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumzia kifo hicho kilichotokea leo tarehe 22 Julai 2019, Mustafa Aboud Juma, Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Usafirishaji visiwani Zanzibar amesema, mpaka sasa hakuna taarifa zozote za chanzo cha kifo hicho.

“Hatujajua chochote mpaka sasa, hatuelewi sababu za kujinyonga,” amesema Juma.

Mhandisi huyo alijinyonga wakati meli hiyo ikitoka Unguja kwenda Pemba na kwamba, baada ya taarifa za kifo hicho, meli hiyo ilisitisha kuendelea na safari na kurudishwa Unguja.

Taarifa zaidi zinaeleza, Injinia Khatib (55) alijinyonga akiwa kwenye chumba cha injini ambamo ndio muda wote hufanyia kazi zake.

Akizungumzia utendaji wa injinia huo, Juma amesema injinia huo alikuwa ni mzowefu na aliyefanya kazi hizo kwa muda mrefu na weledi mkubwa.

Hata hivyo ameeleza, Jeshi la Polisi visiwani humo limeanza kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *