Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge kutokuwa ‘live’: Spika Ndugai ataja ‘mchawi’
Habari za Siasa

Bunge kutokuwa ‘live’: Spika Ndugai ataja ‘mchawi’

Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge amesema, miongoni mwa sababu za Bunge hilo kutorushwa ‘live’, wabunge wenyewe kutojiheshimu. Anaripoti Dandon Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo tarehe 13 Juni 2019, Spika Ndugai amesema kuwa, baadhi ya vitendo vya wabunge hao, vimekuwa vikitia aibu mhimili huo.

“Kuna baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakipiga kelele wakati wa mijadala muhimu kuhusu masilahi ya nchi,” amesema wakati akiwataka wabunge kuwa wasikivu na watulivu wakati Waziri wa Fedha na Mipango, atakapoisoma bajeti mpya ya serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 leo jioni.

“Wengi huwa mnaandika, mnalalamika kwamba kwanini bunge ‘live’ hakuna. Moja ya sababu ni hii hali, ndiyo ukweli wenyewe.

“Unapoonesha ‘live’ hii hali ambayo spika kila wakati anawaambia wabunge tusikilizane, yani nyie wenyewe hamuwezi kusikiliza kila mmoja akaona, ni aibu kubwa,” amesema Spika Ndugai.

Kiongozi huyo wa Bunge amesema, “kwa mfano, hotuba ya leo itasomwa Afrika Mashariki nzima, na hakika mkiweza kuangalia mabunge yote, mtaona utulivu ni tofauti kabisa.

“Kwa wenzetu wanasikiliza, sisi kwetu watu hawana habari, sijui kwa sababu takwimu zinasomwa hapa, unajua si wote wanaweza kuvumilia hesabu.”

Spika Ndugai amewataka wabunge kuwa na desturi ya kuheshimu mijadala ya bunge na kuisikiliza kwa makini, ili waweze kuchangia vyema mijadala hiyo.

“Tuwe na utulivu, watu wanashangaa hili bunge ni la aina gani! watu wanapiga michapo wanageuka nyuma, mwengine anakaa saa nzima anaongea na mwingine, wengine mnawabughuzi wanashindwa kusema ondoka,” amesema Spika Ndugai na kuongeza:

“Serikali inaleta taarifa serious, tuonekane tunaisikiliza taarifa hiyo, nawaombeni tujenge utamaduni wa kusikiliza vitu ili wakati wa kuchangia uchangie kutokana  na taarifa halisi ulizonazo, kuliko unakuja kivyako kwa sababu hujasikiliza.”

Aidha, Spika Ndugai amewaonya wabunge watakaofanya fujo siku ya leo kwamba, atataja majina yao hadharani ili wananchi wao wajue wanachokifanya bungeni.

“Kutembea tembea haipendezi kwa kweli, jioni nitakachofanya nitakua nataja majina tu kwa sababu nina uhakika nchi nzima watakua wanaangalia,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!