Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa JPM akerwa wabunifu umeme kutosaidiwa
Habari za Siasa

JPM akerwa wabunifu umeme kutosaidiwa

Spread the love

RAIS John Magufuli ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco), kushindwa kuwasaidia John Mwafute na Jairos Ngairo ambao ni wabunifu wadogo wa mitambo ya kufua umeme. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Rais Magufuli ameeleza hayo leo tarehe 13 Juni 2019, baada ya Mwafute na Ngairo kumlalamikia kwamba, wamekosa msaada kutoka Tanesco hivyo kushindwa kuimarisha ubunifu huo.

Baada ya kusilikiliza maelezo ya wabunifu hao, Rais Magufuli alitaka kusikia kauli ya Dk. Tito Mwinuka, Mkurugenzi wa Tanesco kutokana na kuwekea vikwazo wabunifu hao ambao wangeweza kulisaidia taifa kwenye uzalishaji nishati hiyo.

“Ninyi watu wa Tanesco mnajisikiaje unaenda mahali, palikuwa giza halafu baadaye unakuta taa zinawaka, huwa unajiulizaje?” amesema Rais Magufuli.

Akitoa ufafanuzi wa malalamiko hayo, Dk. Mwinuka amemueleza Rais Magufuli kwamba, hajawahi kupata taarifa za undani juu ya wabunifu hao na kuwa, mpango wa kuwasidia wabunifu hao upo.

“Nianze kukiri kwamba,.. taarifa za kuwepo kwa wabunifu hawa tumezipata sio muda mrefu. Tanesco tumekuwa tukijihusisha zaidi na wazalishaji wadogo lakini hawa wabunifu sina taarifa kama tumewasadia,” amesema DK Mwinuka.

 Awali, wabunifu hao waliobuni umeme katika Kijiji cha Msete na Kugenge mkoani Njombe ambapo waligunduliwa kupitia kipindi cha Hadubini kinachorushwa kwenye Televisheni ya Taifa (TBC), wameeleza moja ya changamoto zao ni kukosa ushirikiano kutoka Tanesco.

Na kuwa, changamoto huo imesababisha kusitisha ufuaji umeme huo kwa kile walichowaeleza kuwa, hawajapata kibali cha Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

Wabunifu hao wamemueleza Rais Magufuli kuwa, walifanya ubunifu huo kutokana na changamoto za nishati na maji zilizokuwa zikiwakabili wao na wananchi wengine.

Mwafute ameeleza kuwa alianza ubunifu huo mwaka 1980, baada ya kuchagizwa na ukosefu wa betri za radio,  ndipo  alipoanza kubuni umeme wa kienyeji ambapo mwaka 2003, Wajerumani walivyoona ubunifu huo, walimsaidia kwa kumpa nguzo, vikombe, nyanya na mafunzo.

 Anasema, ilipofika 2005 alianza ujenzi wa umeme rasmi na mwaka 2007 alipata ajali, na kwamba ilibidi ajiuguze na baadaye mwaka 2009, aliwasha umeme ambao haukuwa na matumizi makubwa.

Hivyo, alikwenda kwenye maporomoko makubwa ya maji katika kijiji kingine na kufanikiwa kuzalisha Megawati 400 za umeme unaotumika kwenye Kijiji cha Lilondo.

Licha kuzalisha umeme huo, Mwafute amewezesha upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo na watumiaji wanasema kuwa, matumizi ya umeme huo ni sawa na ule wa Tanesco.

Naye Mzee Ngairo amesema, biashara ya pombe ndiyo iliyompa chachu ya kutengeneza umeme huo mwaka 2007, ambapo aliona ni hasara kutumia jenereta.  Umeme huo ulikuwa na uwezo wa kuwasha nyumba 400.

 Amesema kuwa, aliieleza serikali ya kijiji kuwa watapeleka kwenye zahani na shule za kijiji hicho.

 Ngairo ameeleza kuwa, changamoto inayomkabili ni kukosa nyanya, vikombe na Transformer na kwamba, alipata kikwazo kutoka kwa Meneja wa Tanesco, Mkoa wa Njombe aliyeeleza kuwa, anafanya hayo kinyume cha sheria na kuwa, hawajapata kibari kutoka Ewura.

Ngairo aliyezaliwa 1962, alieleza kuwa mwaka 2007 kijijini kwao kilikuwa na changamoto ya nishati ya betri, ndipo alipoanza harakati za kuzalisha umeme.

“Walifika moafisa wa vitambulisho wa vya Taifa (NIDA), waliokuja kuandikisha wananchi vitambulisho, walipata changamoto ya nishati ili kufanya kazi zao za kupiga picha wananchi, nikawapa nyumba na umeme wangu ambapo walipomaliza walitaka kunilipa, nami sikuona haja ya kulipwa.

“Ndipo walipomueleza Mkuu wa Mkoa, naye aliniita na kunikutanisha na Meneja Tanesco wa Mkoa wa Njombe, ndipo alipoambiwa yupo vizuri ila uwezo wake mdogo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!