April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mapato ATCL yaongezeka

ATCL Dreamliner

Spread the love

MAPATO ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), yameongezeka kutoka Sh. 11.7 Bilioni mwaka 2015/16 hadi Sh. 45.5mwaka 2018/19. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Hayo yamesemwa Dk. Phillip Mpango leo tarehe 13 Juni 2019, wakati akielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu, kuanzia mwaka 2016/17 mpaka 2018/19.

Dk. Mpango amesema, mafanikio hayo yametokana na hatua ya Rais John Magufuli kuboresha utendaji wa ATCL, ikiwemo kuongeza idadi ya ndege.

“Uboreshaji huo imesaidia kuongezeka mapato ya ATCL kutoka Sh.11.756 Bil. hadi 45.5632 Bil. Hivi karibuni ATCL,” amesema Dk. Mpango.

Vile vile, Dk. Mpango amesema idadi ya abiria imeongezeka kutoka 49,854 mwaka 2015/16 hadi 242,668 mwaka 2018/19. Pia, miruko (flights) imeongezeka kutoka 672 hadi 3808 mwaka 2018/19, pamoja na idadi ya vituo kutoka kimoja hadi vitano.

Mafanikio mengine aliyotaja Dk. Mpango ni ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge, uboreshaji na ufufuaji wa njia ya reli, ununuzi wa vichwa vya treni 11 vitakavyotumika katika njia kuu na mabehewa 15.

Vile vile, Dk. Mpango amesema mafanikio mengine ni uboreshaji wa huduma za afya kufuatia ujenzi wa hospitali, zahanati, vituo vya afya, na upatikanaji wa dawa za kutosha katika hospitali za umma.

error: Content is protected !!