Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Upinzani watangaza ‘vita’ mpya
Habari za Siasa

Upinzani watangaza ‘vita’ mpya

Hashimu Rungwe
Spread the love

VYAMA vinane vya upinzani nchini, vimedhamiria mambo mawili makubwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani. Anaripoti Hamisi Mguta … (endelea).

Vyama hivyo vimedhamiria kufungua keshi ya kudai Tume Huru ya Uchaguzi na pili, kumfunguia mashitaka Adelardus Kilangi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa madai ya kupotosha umma.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 22 Mei 2019 na Hashim Rungwe, mwenyekiti wa umoja huo mbele ya wanahabari wakati akiipongeza Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kuzuia wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na jiji nchini kusimamia chaguzi.

“Sio kwamba tunaishia hapo, tunakwenda mbali zaidi. Tunataka Tume Huru ya Uchaguzi kwasababu bila hivyo, itakuwa ni miujiza kwa watu wa upinzani kutangazwa.

“Hatutegemei kama tutatangazwa na hawa watu, tunajipanga kwenda kudai haki ili tupate Tume Huru ya Uchaguzi,” amesema Rungwe huku akitoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa na wasimamizi wake uchaguzi.

Miongoni mwa vyama vinavyounda umoja huo ni pamoja na NCCR Mageuzi, NLD, Chadema, CHAUMMA na ACT Wazalendo.

Rungwe amesema, “Kutokana na maamuzi haya yanayoilazimisha NEC kuwa na watendaji wake wa kusimamia uchaguzi, huu ni wakati muafaka kwa wakurugenzi nao kusimamiwa na NEC.”

Rungwe amesema, umoja huo utaendelea kupigania mchakato wa upatikanaji Katiba Mpya itakayoweka mazingira sawa katika uchaguzi.

“Katiba Mpya itaondoa mzizi huu wa fitina, kuna vitu vina udhi, vinatia kichefuchefu lakini utafanyaje?” amesema.

Rungwe amabaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) amesisitiza dhamira ya kumshitaki Kilangi kwa madai ya upotoshaji kuhusu hukumu ya wakurugenzi kutosimaia uchaguzi iliyotolewa na Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.

“Sasa tunakabiliwa na propaganda za kupotosha kuhusu haya yaliyoamuliwa na mahakama kuu. Kumekuwepo na jitihada za CCM na serikali kupotosha maamuzi halali ya mahakama.

“Kwanza kuhusu utekelezaji wa hukumu yenyewe, inajaribu kujengwa picha kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ikisema yeye amekata rufaa hivyo hukumu itasimama hadi rufani itakapoamuliwa, “ amesema Rungwe.

Rungwe ambaye Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania amesema, “ukikata rufaa au ukipata ushindi kwenye ile rufaa kama ulifungwa, unatolewa nje na ukikata rufaa, ukishindwa utarudishwa ndani.

“Sio mtu akikata rufaa hukumu inaisha, AG anajenga picha ya kupotosha wananchi kwamba, hukumu itasimama, hukumu haitasimama.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Wanaotaka kujifunza ZEC kwao kukoje?

Spread the loveMKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Biteko, Nape wanadanganya?

Spread the loveKWA mila na desturi zetu za Kiafrika mkubwa huwa hakosei,...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miamka 60 ya Muungano: Tunakwama wapi?

Spread the loveRAIS wa Jamhuri, Samia Suluhu Hasssan, Ijumaa iliyopita, aliongoza mamilioni...

error: Content is protected !!