Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Madeni ya Simba yakwamisha Bil. 20 za uwekezaji wa MO
Michezo

Madeni ya Simba yakwamisha Bil. 20 za uwekezaji wa MO

Spread the love

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ amesema kuwa madeni ndiyo sababu kuu iliyopelekea pesa za uwekezaji Sh. 20 bilioni kushindwa kufika ndani ya klabu hiyo mpaka pale mahesabu yatakapokamilika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mwekezaji huyo amesema kuwa wakati wanafanya mabadiliko ya muundo wa klabu hiyo waligundua kuwa klabu hiyo ilikuwa na madeni mengi ya siku za nyuma ambayo mengine hayakuwa na maelezo yakutosha licha ya kukubali kuyalipa kama walivyokubaliana.

“Ukitaka kufanya mabadiliko kwanza lazima tuwe na mahesabu yaliyokamilika, ambayo sasa tumeyakamilisha, la pili tulikubaliana na Simba kuwa tutachukua mali na madeni ya klabu ya Simba kama majengo, uwanja wa Bunju lakini pia Simba ina madeni ya TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania).

“Sasa hauwezi kufanya mabadiliko kabla hatujafanya mahesabu na hesabu hizo siyo za mwaka mmoja ni hesabu za miaka mitatu lakini hayo yamesha kamilika,” alisema MO.

Lakini aliongezea kuwa kuwa pesa hizo zipo tayari na alishawajulisha kwa maandishi na ameshaanza kufanya uwekezaji kwa miaka miwili toka aliposhinda zabuni ndani ya klabu hiyo Desemba 3, 2017.

Ikumbukwe klabu hiyo ilibadilisha mfumo wa uwendshaji na timu hiyo kuendeshwa kwa mfumo wa hisa baada ya wanachama wa klabu hiyo kuridhia kwa kufanya marekebisho kwenye katiba yao ya hapo awali.

Simba ambayo jana ilifanikiwa kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Tazama video kamili hapo chini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!