Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli kukata mzizi wa fitina kikokotoo cha mafao
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli kukata mzizi wa fitina kikokotoo cha mafao

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli leo tarehe 28 Desemba 2018 atakutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii na mawaziri wa wizara husika, kwa ajili ya kujadili masuala yahusuyo mafao ya wafanyakazi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli pia atazungumza na viongozi hao kuhusu kanuni mpya ya kukokotoa mafao ya wastaafu.

Vyama vitakavyokutana na kuzungumza na Rais Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam, ni pamoja na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA), vyama shiriki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSD na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA).

Kanuni mpya ya kikokotoo iliyotolewa hivi karibuni na serikali, ambayo inaelekeza wastaafu kulipwa mkupuo wa asilimia 25 ya mafao pindi watakapostaafu na asimilia 75 inayobaki watakuwa wakilipwa kama pensheni ya kila mwezi.

Baada ya kikokotoo hicho kutangazwa kwa umma, baadhi ya vyama vya wafanyakazi ikiwemo TUCTA, viliipinga kanuni hiyo kwa maelezo kwamba inakandamiza wafanyakazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!