March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sekta binafsi yapigilia msumali sakata la Fastjet

Spread the love

MKURUGENZI wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye ametoa neno kuhusu madai yaliyotolewa na baadhi ya watu hivi karibuni, ya kwamba Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) inaibeba Kampuni ya Ndege ya Taifa (ATCL), akisema kuwa mamlaka hiyo haipendelei mtu bali inafuata sheria. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kuali hiyo ya Simbeye imekuja katika kipindi ambacho kuna vuguvugu la Shirika la Ndege la Fastjet kuzuiwa kufanya baadhi ya shughuli zake na TCAA kwa sababu mbalimbali ikiwemo kudaiwa madeni, ambapo baadhi ya watu waliibuka na kuihusisha hatua hiyo kwamba imelenga kuidhoofisha shirika hilo na kuibeba ATCL.

Akizungumzia kuhusu madai hayo, Simbeye  amesema TCAA haiipendelei ATCL bali inafuata sheria kwa kuwa ilishawahi kuifungia ATCL ilipokiuka sheria.

Hata hivyo, Simbeye ameshauri kuwa, TCAA ifuate sheria bila kukandamiza mtu kwa kuwa serikali inahitaji kushirikiana na watu binafsi katika usafiri wa anga.

“Nimeridhika kwamba sio TCAA wanaipendelea ATCL hapana ni kwamba wao wanafuata sheria, nimefarijika kiwamba hata ATCL ilishawahi kufungiwa na wao ni shirika la serikali, hawa watu wako ‘fair’ wanafuata sheria, na waendelee kufuata sheria bila kumkandamiza mtu yeyote, serikali inahitaji kushirikiana na watu binafsi katika usafiri wa anga,” amesema na kuongeza.

“Kama kuna mahali ya kuwasaidia wazawa hata kama ushauri wa maneno wasiache kuwapa kama ambavyo wanasema wameshawapatia waendelee kuwapa ushauri hatua kwa hatua, jambo lililojitokeza wapewe uashauri namna ya kufanya, TCAA itekeleze sheria na lakini pia iweze kuwasaidia kutoa ushauri hawa ni wazawa wanahitaji kusaidiwa kuliko wa nje.”

error: Content is protected !!