February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Shabiki apoteza maisha uwanjani

Spread the love

SHABIKI wa Inter Milan amepoteza maisha na wengine wanne kujeruhiwa katika mchezo dhidi ya FC Napol uliopigwa kwenye uwanja wa San Siro baada ya kuibuka vurugu kubwa kwa mashabiki wa pande zote mbili kabla ya mechi.

Taarifa kutoka nchini Itaria zinasema kuwa mshabiki huyo alipoteza maisha kwa kugongwa na gari nje ya uwanja kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliocheza jana na kushuhudia Inter Milan kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Napol.

Katika mchezo huo ambao uligubikwa na vurugu nyingi ndani na nje ya uwanja kiasi cha kupelekea beki wa kati wa klabu ya Napol anaye windwa na Manchester United, Kalidou Koulibaly kutolewa nje ya uwanja baada ya kuoneshewa kadi mbili za njano.

Licha ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa mchezaji huyo, mashabiki wa wa Inter Milan walionekana kufanya vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa beki huyo baaada ya kutoa milio kama nyani wakati mchezaji huyo anaposhika mpira uwanjani kiasi kilichompelekea kuandika ujumbe mzito katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Vitendo hivyo ambavyo Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kuvipinga vikali lakini bado vinaonekana kushamili kwa wachezaji wenye ngozi nyeusi wanaocheza soka la kulipwa barani Afrika.

error: Content is protected !!