Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Matokeo darasa la saba yatangazwa, ufaulu waongezeka
ElimuTangulizi

Matokeo darasa la saba yatangazwa, ufaulu waongezeka

Spread the love

WATAHINIWA 733,103 kati ya 943,318 wamefaulu mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi wa mwaka 2018. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akitangaza matokeo hayo leo tarehe 23 Oktoba 2018 jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde  amesema  ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 4.96 kutoka asimilia 72.76 kwa mwaka jana hadi kufikia 77.725 mwaka 2018.

Dk. Msonde amesema takwimu zinaonyesha kuwa ufaulu katika masomo ya Maarifa ya Jamii, Kiingereza, Sayansi na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.03 na 11.92 wakati somo la Kiswahili ukishuka kwa asilimia 1.44 ikilinganishwa na ufaulu ulivyokuwa mwaka 2017.

Katika hatua nyingine, Dk. Msonde amesema kati ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo, wasichana walikuwa 383,830 idadi ambayo ni sawa na asilimia 77.12 na wavulana 350,273 (78.38)

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!