February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Usafiri wa meli kutoka Dar- Z’bar wasitishwa

Spread the love

USAFIRI wa majini kati ya Dar es Salaam na Zanzibar umesitishwa siku ya leo hadi hapo utakapotangazwa tena. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kampuni ya Azam Marine na Kilimanjaro Fast Ferries kwa kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA) pamoja na taarifa kutoka Mamlaka Ya Udhibiti wa Hali ya Hewa (Zanzibar) imetangaza kusitisha safari hizo kutokana na hali mbaya ya hewa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa safari huzo zimesitishwa kuanzia leo tarehe 23 Oktoba, 2018 kutokana na hali ya hewa mpaka itakaporuhusiwa na mamlaka husika pamoja na hali baharini kutulia.

Abiria waliokuwa wanatakiwa kusaifiri siku ya leo watembelea ofisi za Azam Marine kwa maelezo zaidi.

error: Content is protected !!