March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tisa mbaroni kwa mauaji ya watoto wa familia moja

Pingu

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu tisa wanaoshukiwa kuhusika na tukio la kuwauwa kinyama watoto wawili wa familia moja na kuwatupa kichakani kwenye kijiji cha Mashule wilaya ya Bukoba. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wanahabari mapema leo tarehe 23 Oktoba 2018, Kaimu Kamanda wa Polisi Kagera, Issack Msengi ameeleza kuwa, mauaji ya watoto hao, Auson Respikius (7) na Alistidia Respikius (5) yanahusishwa na imani za kishirikina.

“Mauaji haya ya watoto yanahusishwa na imani za kishirikina na mpaka sasa tunawashikilia watu Tisa kuhusiana na tukio hilo,” amesema Kamanda Msengi.

Kwa mujibu wa Baba wa watoto hao, John Respikius anadai kuwa watoto wake walipotea tangu Jumapili tarehe 21 Oktoba 2018 ambapo jana miili yao ilipatikana kichakani ikiwa imechinjwa.

error: Content is protected !!