Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dodoma ‘walilia’ chakula
Habari Mchanganyiko

Dodoma ‘walilia’ chakula

Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa
Spread the love

RICHARD Kapinye, diwani wa kata ya Kibaigwa na Mwenyekiti wa kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira ya halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ameiomba serikali ya Rais John Magufuli kuagiza chakula kwenye mfumo wa soko ili kupunguza bei ya nafaka hususan mahindi, anaandika Dany Tibason.

Kapinye alitoa kauli hiyo katika kikao cha baraza la madiwani wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.

Amesema serikali ikiingiza chakula sokoni na kuuza angalau debe kwa sh.10,000/= waliohifadhi chakula katika maghala watatoa nafaka na kuziuza kwa bei nafuu ili wananchi waweze kumudu kununua nafaka hizo.

“Bei ya mahindi kwa debe moja kwa sasa ni kati ya Sh. 20,000/= hadi 22,000/= katika maeneo mengi wilayani Kongwa na mvua imeanza wiki hii” amesema Kapinye.

Pamoja na ombi la kamati hiyo kwa serikali, Deogratias Ndejembi Mkuu wa Wilaya hiyo amesisitiza wananchi kujikita katika kilimo cha mtama na mazao mengine yanayostahimili ukame kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Katika kikao hicho Chilingo Chimeledya, mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ambaye pia ni diwani wa kata ya Sejeli alitoa shukrani kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msaada wa madawati 997 Katika halmashauri ya Kongwa.

Kamati hiyo imemshukuru Job Ndugai, Mbunge wa Jimbo la Kongwa na spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kufanikisha upatikanaji wa Dola za Kimarekani 10,000/= kutoka ubalozi wa China.

“Fedha hizo zilitumika kununua saruji mifuko 1,557 iliyogawanywa ili kukamilisha ujenzi wa madarasa ya shule yaliyo kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!