August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu akamatwa na Polisi, aletwa Dar

Tundu Lissu, Rais wa TLS

Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria wa Chadema, amekatwa na polisi nje ya Bunge na kupelekwa jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Tukio hilo limetokea leo jioni baada ga Lissu kutoka bungeni lakini haijafahamika mara moja amekamatwa kwa kosa gani.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amethibitisha kukamatwa kwa Lissu lakini hajajua sababu ya kukamatwa kwake.

“Kweli Lissu amekamatwa na kupakiwa kwenye Land Cruiser ya Polisi na kupelekwa Dar, lakini hatujajua amefanya kosa gani,” amesema Mbowe.

MwanaHALISI Online inaendelea kufuatilia tukio hilo na litakujuza kinachoendelea.

error: Content is protected !!