Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Mkuu apokea maoni ya wakazi wa Ngorongoro
Habari Mchanganyiko

Waziri Mkuu apokea maoni ya wakazi wa Ngorongoro

Spread the love

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa jana tarehe 25 Mei, 2022 amepokea mapendekezo kutoka kwa wananchi wa Tarafa za Loliondo, Ngorongoro na Sale kuhusu namna bora ya kulinda uhifadhi wa maeneo hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Maoni hayo yaliwasilishwa kwa Waziri Mkuu na wawakilishi wa wakazi wa wilaya hiyo wakiwemo Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Shangai, Malaigwanani, Madiwani, wenyeviti wa vijiji, wawakilishi wa wanawake na vijana, ofisini kwake Mlimwa, Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Malaigwanani kutoka Tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale wilayani Ngorongoro baada ya kupokea mapendekezo ya mwananchi kuhusu namna bora ya uhifadhi katika tarafa hizo, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 25, 2022. Kulia wake ni Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Sangay na kushoto wake ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Ngorongoro, Ndirango Ole Senge.

Baada ya kupokea mapendezo hayo, Waziri Mkuu aliwasisitiza wananchi hao waendelee kuiamini Serikali yao kwani haiwezi kuwa na mipango mibovu kwa wananchi wake.

“Msisikilize maneno maneno ya watu wa pembeni,” amesema.

Akizungumzia kuhusu eneo la Msomera lililoko wilayani Handeni, Tanga ambako yanaandaliwa makazi kwa ajili ya kuwahamishia wakazi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiari alisema ujenzi unandelea vizuri.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa wanawake kutoka Tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale wilayani Ngorongoro baada ya kupokea mapendekezo ya mwananchi wa Tarafa hizo kuhusu namna bora ya uhifadhi katika tarafa hizo, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 25, 2022. Kulia wake ni Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Sangay na kushoto wake ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Ngorongoro, Ndirango Ole Senge.

Waziri Mkuu amesema ujenzi wa nyumba za makazi 103 upo mbioni kukamilika na pia, Serikali imepanga kuongeza nyumba nyingine lengo likiwa ni kufikia nyumba 500 kwa ajili ya wakazi hao.

Pia Majaliwa amesema Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya mifugo ili kuhakikisha wafugaji wote nchini wanapata tija kupitia shughuli hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!