July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi TLS: Mtobesya atoa ujumbe

Mgombea Urais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Jeremiah Mtobesya

Spread the love

 

SAA chache kupita tangu Profesa Edward Hoseah kutangzwa mshindi wa urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Jeremiah Mtobesya ametoa ujumbe wa shukran na kuhitimisha kampeni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Uchaguzi mkuu wa TLS umefanyika leo Ijumaa tarehe 27 Mei 2022, katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Arusha (AICC) kwa Profesa Hoseah akipata kura 628, Mtobesya akipata kura 145 na Harold Sungusia akipata kura 380.

Baada ya matokeo hayo, Mtobesya ametoa ujumbe wa kuzungumzia mchakato huo na kuhitimisha safari za mbio za kampeni za uchaguzi huo.

Ujumbe huo wa Mtobesya unasema:

Habari za muda huu ndugu zangu!

Naomba niwashukuru sana watu wote waliosimama na mimi katika kipindi hiki cha kampeni, ama kwa kuninadi kwa wapiga kura au kwa kunitia moyo kwa kushiriki katika kinyang’anyiro hiki. Sina cha kuwa lipa, bali ninawashukuru sana!!

Kwa wale wapiga kura 145 walikuwa na imani na mimi na kuamini yale niliyoyasimamia, nawashukuruni sana kwa imani yenu kwangu japokuwa kura hazikutosha kuniwezesha kushinda uchaguzi.

Kwa wagombea wenzangu, niwashukuru wote kwa kampeni ambayo nadhani tangu chama chetu kianzishwe miaka mingi iliyopita, hakujawahi kutokea kampeni ya namna hii ambapo kulikuwa na ushindani wa hali ya juu na kila mtu akijaribu kunadi sera zake kwa wapiga kura kwa namna ambayo aliamini inaweza kumpatia ushindi siku ya uchaguzi.

Kwa wasomi wenzangu ambao tulikuwa kwenye makundi matatu yaliyokuwa yakiwaunga mkono wapiga kura, yawezekana katika kipindi hiki cha wiki sita za kampeni tulikwazana na kukwaruzana kwa namna yoyote ile, naomba tuweke tofauti zetu pembeni tukijenge chama chetu!

Mwisho kabisa nimpongeze Prof. Edward G. Hoseah kwa kuchaguliwa tena kukiongoza chama chetu kwa mwaka 2022/2023.

Asanteni sana na nawatakia jioni njema!!!

Jeremiah Mtobesya
Mgombea Urais wa TLS 2022/2023

error: Content is protected !!