July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ni Profesa Hoseah tena TLS

Dk. Edward Hoseah, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)

Spread the love

 

PROFESA Edward Hoseah kwa mara nyingine amechaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS). Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea)

Ni katika uchaguzi mkuu uliofanyika leo Ijumaa tarehe 27 Mei 2022, ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Profesa Hoseah aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) amewashinda mawakili wenzake aliokuwa akichuana nao, Harold Sungusia na Jeremiah Mtobesya.

Katika uchaguzi huo, Profesa Hoseah amepata kura 621, Mtobesya 145 na
Sungusia 380

Hii itakuwa awamu yake ya pili mfululizo kuongoza chama hicho cha wasomi.

error: Content is protected !!