November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Aweso aeleza mikakati kumaliza mgawo wa maji Dar

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imepanga kutumia zaidi ya Sh.390 bilioni kujenga bwawa la kuhifadhia maji katika Kijiji cha Kidunda wilayani Morogoro vijijini mkoani Morogoro. Anaripoti Danson Kaijage, Morogoro … (endelea).

Ujenzi huo una lengo la kuweka akiba ya Mto Ruvu ambao ni chanzo kikubwa cha huduma ya Maji kwa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.

Bwawa hilo linategemea kuwa na urefu wa mita 860 na kimo cha mita 21 na uwezo wa kuhifadhi maji lita billioni 190.

Maji hayo kwa sehemu kubwa husababisha mafuriko wakati wa mvua za masika hivyo yakihifadhiwa kwenye bwawa hilo la yatasaidia tatizo la upatikanaji wa maji wakati wa kiangazi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, mara baada ya kutembelea ili kuona na kujiridhisha eneo la utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati.

Mbele ya waandishi wa habari, Waziri Aweso amesema Serikali imeshalipa fidia ya Sh.12 billioni kwa wananchi wa eneo la Kidunda waliopisha ujenzi wa bwawa hilo na tayari wananchi wameshaondoka eneo la mradi ili kupisha ujenzi kuanza.

error: Content is protected !!