Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL
Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the love

WAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education Link (GEL), imewataka wazazi ambao watoto wao wamekosa nafasi za kusoma vyuo vikuu  ndani ya nchi wasipate mfadhaiko wa moyo na badala yake wafike GEL kwaajili ya kupata nafasi kwenye vyuo vikuu nje ya nchi ndani ya  muda mfupi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa GEL, Abdlulmalik Mollel, wakati akizungumza na wazazi na wanafunzi zaidi ya 100 ambao wanatarajia kusafiri wiki hii kwenda nje ya nchi kuanza mwaka wa masomo.

Alisema wanafunzi hao walielezwa mambo ya msingi ya kuzingatia kabla ya safari, wakati wa safari na hata baada ya kufika kwenye nchi wanazokwenda  hasa kuzingatia masomo na kuachana na biashara zingine ambazo zitawapotezea malengo.

Alisema anafahamu kwamba wanafunzi wengi wanaotaka kusomea  fani za uhandisi na udaktari wamekosa nafasi kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo kwenye vyuo vya ndani lakini hawana sababu ya kupata presha kwani nafasi bado zipo kwenye vyuo mbalimbali nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL) Abdulmalik Mollel, akizungumza na wazazi na walezi wa wanafunzi wanaotarajiwa kwenda nje ya nchi kwa masomo ya fani mbalimbali

“Tunafahamu kwamba wanafunzi wengi hasa wa masomo ya uhandisi na fani za afya kama udaktari wamekosa kwasabahu nafasi ilikuwa chache kwa hapa nchini lakini njooni Global Education Link tutahakikisha watoto wenu wanapata nafasi ndani ya muda mfupi uliobaki na watasafiri kwenda kusoma,” vyuo mbali mbali nje ya nchi,” alisema

Aidha, Mollel alisema mbali na kuunganishwa na vyuo vikuu nje ya nchi kwa haraka kwenye mwaka huu wa masomo, wanafunzi ambao watapata changamoto ya ada watapatiwa mikopo isiyo na riba kwaajili ya ada ili wawahi mwaka wa masomo.

“Wazazi mliobahatika kuja hapa leo tunaomba muendelee kutuamini lakini pia muwatangazie wazazi wengi ambao watoto wao wamekosa nafasi za vyuo vikuu Tanzania kwamba ndoto za watoto wao zinaweza kutimia kwani nafasi zipo, waje kwetu tutawapa Visa na tiketi ndani ya muda mfupi, wasikae kinyonge wakadhani watoto wao wamekwama kabisa,” alisema

Wazazi na wanafunzi wanaotarajiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kwa masomo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL) Abdulmalik Mollel, alipokutana nao kuwaasa kuhusu mambo ya kuzingatia watakapokuwa nje ya nchi kwa masomo

“Wazazi lazima watambue kwamba mtoto wako anaweza kuwa amepata daraja la kwanza lakini anazidiwa point na wenzake waliochukuliwa kwenye vyuo vya hapa nchini lakini hiyo haimaanishi kwamba amefeli, amekosa nafasi kutokana na ushindani uliokuwepo kwa hiyo njooni GEL tuwaunganishe na vyuo vya nje ya nchi nafasi bado zipo wataenda kusoma,” alisema Mollel

Aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu ni watu wazima wanaotakiwa kuanza kutatua changamoto watakazokutana nazo kwa kuwasiliana na maofisa wa vyuo vikuu walivyopo au maofisa wa Global na kuachana na kasumba ya kuwasumbua wazazi wao  kwa kila jambo ambalo wanaona haliko sawa.

“Unakuta mwanafunzi kaona mende chumbani kwake anapiga picha anamrushia mzazi wake sasa unataka mzazi wako atasafiri kuja China kuondoa mende? Ukiwa mwanafunzi wa chuo kikuu ni mtu mzima unayeweza kukabiliana na changamoto kwa hiyo siyo kila kitu unamwambia mzazi wako. Kama umekuta chumba ni kichafu safisha, kama umekuta mende muondoe mende siyo unamwambia mzazi wako,” alisema Mollel.

Alisema kwa mwaka huu wa masomo Global Education Link inatarajia kusafirisha zaidi ya wanafunzi 1,500 kwenda kusoma vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi na kuahidi kuwa wengine watakaojitokeza watapatiwa nafasi za kwenda kwenye vyuo vikuu mbalimbali kwani ushindani vyuo vya ndani umekuwa mkubwa na wengi wao wamekosa nafasi.

“Udahili wa vyuo vikuu vya ndani umefikia ukingoni, dirisha la pili limefungwa dirisha la tatu litafungwa tarehe 29 mwezi huu inawezekana kukawa na kundi kubwa linataka kusomea udaktari wa meno, moyo, mama cheza au zozote zile kama uhandisi kama kuna mwanafunzi amekosa kozi ya yoyote ya sayansi mwanafunzi asihisi amechelewa aje Global  au apige simu hii 0656200200 atapata nafasi nje ya nchi,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

error: Content is protected !!