Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Putin aita vikundi vya kujitolea vita ya Ukraine
Kimataifa

Putin aita vikundi vya kujitolea vita ya Ukraine

Spread the love

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, amefungua milango ya ushirikiano kwa vikundi vya kijeshi vya kujitolea ,ili kuongeza nguvu katika vita kati yake na Ukraine. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Ripoti hiyo imetolewa na Andrei Troshev, msaidizi wa zamani wa aliyekuwa kiongozi wa Kundi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, aliyefariki dunia kwa ajali ya ndege miezi michache baada ya kutangaza uasi dhidi ya Serikali ya Putin.

Mtandao wa BBC Swahili umeripoti kuwa, Putin alitangaza uamuzi wa kushirikiana na vikundi vya kujitolea katika vita nchini Ukraine, wakati akizungumza na Troshev.

Troshev alisema Putin ameahidi kushirikiana na vikundi hivyo katika operesheni mbalimbali za kijeshi “unajua masuala ambayo yanahitaji kutatuliwa mapema ili mipangilio katika eneo la mapigano iende kwa njia bora na yenye mafanikio.”

Msemaji wa Serikali ya Urusi, Dmitry Peskov, alisema Troshev ambaye zamani alikuwa katika kundi la Wagner, amepewa nafasi katika Wizara ya Ulinzi.

Hayo yanajiri ikiwa umepita mwezi mmoja tangu Putin atoe wito kwa wanajeshi wa Wagner na wa vikundi vingine binafsi kula kiapo cha utii kwa Serikali yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Sakata la uhamiaji Rwanda lamng’oa waziri Uingereza

Spread the loveWaziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Robert Jenrick amejiuzulu baada ya...

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

error: Content is protected !!