WATU takribani 50 wamefariki dunia huku wengine 50 wakijeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea karibu na msikiti nchini Pakistan, wakati wakisherehekea sikukuu ya maulidi ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili, Jeshi la Polisi nchini humo limetaja chanzo cha mlipuko huo ni tukio la kujitoa mhanga lililolengwa katika mkusanyiko wa kidini.
Kufuatia tukio hilo lililotokea katika mji wa Mastung leo Ijumaa, vyombo vya usalama Pakistan, vimetangaza hali ya hatari.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan, Sarfraz Bugti, amelaani tukio hilo akisema ni la kuchukiza.
Mitandao ya kimataifa imeripoti kuwa, Naibu Inspekta wa Polisi wa Pakistan, Munir Ahmed, amedai mlipuaji bomu alilitekeleza tukio hilo karibu na gari ya polisi.
Imeelezwa kuwa, hadi sasa hakuna kikundi cha kigaidi kinachohusishwa na tukio hilo.
Leave a comment