Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko DPP atuma salamu kwa mafisadi, wahujumu uchumi
Habari Mchanganyiko

DPP atuma salamu kwa mafisadi, wahujumu uchumi

Spread the love

MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu, amewataka watumishi wa umma wanaofanya makosa ya rushwa, uhujumu uchumi na ufisadi, waache mara moja kwa kuwa vitendo hivyo vinaathiri ustawi wa jamii. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Mwakitalu ametoa wito huo leo tarehe 29 Septemba 2023, akifungua kikao kazi cha taasisi za haki jinai (Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), jijini Dodoma.

Mkurugenzi huyo wa mashtaka amesema ofisi yake itashirikiana na ofisi za DCI na TAKUKURU, kuhakikisha inawachukulia hatua watu watakaobainika kufanya vitendo hivyo.

“Makosa ya rushwa na uhujumu uchumi na ufisadi yana athari kubwa sana kwa jamii yetu. Yanaongeza gharama za maisha lakini yanasababisha wananchi wakose huduma ambazo walipaswa kuzipata, lakini nafahamu madhara ya makosa mengine ya jinai kusipokuwa na amani na utulivu hakuna mtu atakwenda kufanya shughuli za maendeleo,” amesema Mwakitalu na kuongeza:

“Leo tuko hapa kuweka mikakati ya kukabiliana na vitendo hivyo ili kukomesha uhalifu nchini.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi (CP),Salum Handun, amesema taasisi yake itaendelea kushirikiana na vyombo vingine kwa ajili ya kushughulikia wahalifu.

“Kwa upande wa jeshi kwenyewe ushirikiano umeimarika, tumeanza kushirikiana katika eneo la makosa ya mtandao, kutafuta watuhumiwa na kuwakamata,” amesema CP Hamduni.

Naye DCI Ramadhan Kingai, amesema kikao hicho kitapitia taarifa za utekelezaji wa maazimio ya kikao kilichopita kwa ajili ya kutathimini kazi zao na kuweka mikakati kwa ajili ya mwaka ujao wa 2023/24.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!