SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu wenye ulemavu nchini kupitia fursa ya uwakala na uuzaji wa mkaa mbadala wa Rafiki briquettes.
Mkaa huo ambao ni rafiki wa mazingira unasaidia kuunga mkono juhudi za serikali kukabilina na mabadiliko tabianchi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea)
Mkurugenzi wa Shirika la Foundation For Disabilities Hope (FDH), Michael Salali, amebainisha hayo leo tarehe 27 Septemba 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fursa hiyo.
Amesema shirika la STAMICO, limeanzisha utengenezaji wa mkaa mbadala ambao unafahamika kwa jina la Rafiki briquettes, ambapo watu wenye ulemavu watapatiwa fursa ya kuwa mawakala na wauzaji wa bidhaa hiyo.
“Tunalishukuru sana shirika la STAMICO kwa fursa hii kwa watu wenye ulemavu ambayo inakwenda kusaidia kuwakwamua kiuchumi.
“Kama mnavyofahamu watu wenye ulemavu nchini uchumi wao bado ni duni sana hivyo fursa hii itasaidia kuboresha maisha yao na kuwaondolea changamoto ya unyanyapaa wanaokumbana nao katika jamii zao”amesema
Pia, amesema mkaa huo mbadala utasaidia kuendeleza juhudi za serikali na dunia kwa ujumla katika kukabilina na tatizo la mabadiliko tabia ya nchi yatokanayo na uharibifu wa mazingira kwa kukataji miti hovyo.
“Kama mnavyofahamu dunia ipo katika mapambano dhidi ya mabadiliko tabia nchi lakini pia uharibifu mazingira ambao unachangia watu wenye ulemavu wa ngozi kupata saratani ya ngozi kutokana na mionzi ya jua inayosababishwa na ukosefu wa vimvuli… yote hayo yanatokana na ukataji miti kiholela unaendelea nchini” amesema
Aidha, ametoa wito kwa watu wenye ulemavu nchini kuchangamkia fursa hiyo adhimu ili kujikwamua kichumi na kuacha kuendelea kuwa tegemezi.
Leave a comment