Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watano watupwa jela miaka saba kwa wizi wa pombe
Habari Mchanganyiko

Watano watupwa jela miaka saba kwa wizi wa pombe

Spread the love

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mbozi imewahukumu watu watano kifungo cha miaka saba jela kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya kuvunja na kuiba pombe za aina mbalimbali pamoja na Tv flat screen, mali hizo zikiwa na thamani ya Sh 2,641,000. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea)

Akisoma hukumu hiyo juzi Alhamis, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Chami Changwe aliwataja watu hao ambao ni watuhumiwa hao ambao ni wakazi Vwawa mkoani Songwe,  kuwa ni Michael Nzunda, Samson Sichala, Allen Lwinga, Asheli Mlawizi na Steve Sanga.

Amedai watuhumiwa hao walikiri kufanya kosa hilo tarehe 4 Machi 2023 katika grocery iliyo maeneo ya Vwawa kati wilayani Mbozi.

Watuhumiwa hao walikamatwa maeneo maeneo tofauti tofauti mwaka 2023 ndani ya mkoa wa Songwe, na kuwekwa rumande na juzi hukumu hiyo imetolewa kwa kila mmoja kutumikia kifungo cha miaka saba gerezani.

Wakizungumzia hukumu hiyo, nje baadhi ya wakazi wa Mbozi, Anne Mwashambwa amesema mahakama imetenda haki kwani wezi hao wanarudisha nyuma maendeleo ya watu hasa ikizingatiwa wajasiriamali wengi wapo kwenye ‘mikopo umiza’.

Naye Baraka Mwashihuya ambaye ni mkazi wa Ichenjezya, amesema kutokana na hukumu hiyo, watu wenye tabia za udokozi wataingiwa hofu kujiingiza kwenye wizi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!