Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kigogo ACT-Wazalendo auawa Zanzibar, Polisi wataja chanzo
Habari za Siasa

Kigogo ACT-Wazalendo auawa Zanzibar, Polisi wataja chanzo

Spread the love

ALIYEKUWA Katibu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Jimbo la Chaani, visiwani Zanzibar, Ali Bakari Ali (62), amefariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, baada ya kujeruhiwa na watu wanaodaiwa majambazi, jioni ya tarehe 28 Machi mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Taarifa ya tukio hilo imetolewa leo Jumamosi na Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umm wa Chama cha ACT-Wazalendo, Salim Bimani aliyesema Ali alifariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 29 Machi 2024.

“Tumepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa kitendo cha kutekwa, kushambuliwa na kutupwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kupelekea umauti kwa Ali, mazingira ya kifo chake ni muendelezo wa vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vikitokea katika mji wa Zanzibar na viunga vyake,” amesema Bimani na kuongeza:

“ACT-Wazalendo tunalitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha wanawakamata wahusika wote wa tukio hili la kinyama la kukatisha uhai wa mtu na kuwafikisha wahalifu hao katika vyombo vya sheria.”

MwanaHALISI Online, imemtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Mko awa Kaskazini Unguja, Gaudianus Felician Kamugisha, kubaini undani wa tukio hilo, ambaye amedai Ali hakuuawa na majambazi kama ilivyodaiwa na ACT-Wazalendo, bali amemuawa na watu ambao alikuwa anafahamiana nao.

Kamanda Kamugisha amedai kuwa, Ali ameuliwa na Hamis Nyange Omary (35) akishirikiana na Feisal Makame Hamis (19), baada ya marehemu huyo kushindwa kumlipa fedha alizokuwa anamdai kiasi cha Sh. 1 milioni.

“Watuhumiwa walishambulia kwa kumkata na kitu chenye ncha kali sehemu ya mkono wa kulia na shingoni, chanzo cha tukio hilo ni kwamba Bakari alikuwa hajamlipa Nyange fedha alizokuwa anadaiwa Sh. 1 milioni. Baada ya watuhumiwa kupata taarifa kwamba fedha inataka kulipwa benki wakamfuatilia wakarudi naye kwenye gari mpaka maeneo ya Chaani katika kutolipana ndio wakamfanyia hicho kitendo,” amesema Kamanda Kamugisha.

Kamanda Kamugisha amesema “baada ya kuchoma shingoni wakamtoa kwenye gari wakamtupa chini wakakimbia lakini wanawanchi waliwakimbisha wakachoma gari lakini wao walifanikiwa kukimbia ndipo polisi tulipofika tukampeleka majeruhi hospitali kunusuru maisha yake lakini alifia hospitali.”

Amesema, watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano na ushahidi ukikamilika watafikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!