Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali Z’bar yalaani ukamataji, unyanyasaji kwa wanaokula hadharani wakati wa mfungo
Habari za Siasa

Serikali Z’bar yalaani ukamataji, unyanyasaji kwa wanaokula hadharani wakati wa mfungo

Spread the love

SERIKALI ya Zanzibar, imelaani vitendo vya baadhi ya raia kunyanyaswa kwa madai ya kukiuka taratibu za imani ya dini ya kiislam wakati wa mwezi mtukufu wa mfungo wa  Ramadhan. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Msimamo huo wa Serikali ya Zanzibar, umetolewa na msemaji wake mkuu, Charles Hilary, katika kipindi ambacho kumeibuka mjadala wa wanaokula hadharani wakati wa mfungo wa Ramadhan, kukamatwa na Jeshi la Polisi.

“Serikali inalaani itendo vya unyanyasaji vinavyoendelea kufanyika sehemu mbalimbali Zanzibar, kadhia hiyo ni kinyume na misingi ya kuvumiliana katika imani za kidini.

“Aidha, Serikali inawahimiza wananchi kujizuia kwa namna yoyote ile kuingilia uhuru wa mtu binafsi katika kuabudu,” imesema taarifa ya Hilary.

Taarifa hiyo imesema Zanzibar inaongozwa kwa katiba inayokataza vitendo vinavyohatarisha umoja, amani na mshikamano.

“Ikumbukwe Zanzibar inaongozwa kwa Katiba, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mamlaka ya kuilinda Katiba ya nchi na watu wake, hivyo hatua yoyote ile yenye kuhatarisha umoja, amani na mshikamano haitavumiliwa,” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

“Serikali itaendelea kulinda haki na uhuru wa mtu kuabudu kama ilivyoclezwa katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Zanzibar ni nchi yenye historia kongwe ya uvumilivu wa kidini ambapo Uislamu na Ukristo uliiingia mapema kuwa sehemu muhimu ya utamaduni uliodumu kwa karne nyingi.”

Hivi karibuni Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, liliwakamata watu 12 kwa tuhuma za kukutwa wakila hadharani mchana katika kipindi cha mfungo wa Ramadhan.

2 Comments

  • Mbona haiingii akilini. Anaekamata ni polisi aliyeajiriwa na serikali. Anaelaani ni serikali iliyomwajiri polisi

  • Jambo moja ni uhuru wa kuabudu, jengine ni uhuru wa kufanya uhuni. Uhuru wa kuabudu uwe wa pande zote. Zanzibar tangu zamani ilikuwa ikipinga na kuwaadhibu wanaokiuka maadili ya nchi.
    Ilikuwa anayekamatwa anakula au kulewa hadharani, hufungwa mwaka mmoja na hafunguliwi hadi tarehe kama ile aliyokamatwa. Je taratibu hizi zimebadilishwa?
    Siungi mkono vitendo vya Wananchi kuchukua Sheria mikononi mwao, viachwe vyombo vya dola vifuate taratibu zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!