Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanajeshi Urusi wakwaa kisiki Kiev
Kimataifa

Wanajeshi Urusi wakwaa kisiki Kiev

Spread the love

 

WAKATI mapigano kati ya majeshi ya Urusi na Ukraine yakiingia siku ya nne, taarifa zinaeleza kwamba Urusi imekumbana na upinzani mkali ambao haikuutegemea kutoka kwa majeshi ya Ukraine pale yalipokuwa yakijaribu kupenya kuiingia katika mji mkuu wan chi hiyo- Kiev.

Taarifa za wachambuzi wa masuala ya kivita, zinaeleza kwamba Urusi ilitegemea kuuteka Mji Mkuu wa Kiev kirahisi ndani ya muda mfupi lakini hali inayoendelea kwa sasa inaonesha kwamba majeshi ya Ukraine yanaendelea kupambana vikali kuhakikisha kwamba mji huo hauangukii kwenye mikono ya majeshi ya Urusi na tayari yamefanikiwa kuyarudisha nyuma majeshi ya Urusi ambayo sasa yameelekea katika mji wa Kharkiv.

Mji wa Kharkiv ni mji wa pili kwa ukubwa baada ya mji wa Kiev.

Aidha, taarifa zaidi zinaeleza kwamba mpaka sasa, Urusi imefanikiwa kwa asilimia 50 katika uvamizi huo uliohusisha wanajeshi takribani 150,000 wa Urusi wakiwa na silaha nzito ambapo kutokana na upinzani iliokutana nao kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine, huenda ikaongeza idadi ya wanajeshi katika siku chache zijazo.

Mchambuzi Nigel Gould-Davies kutoka Chuo cha International Institute for Strategic Studies kilichopo jijini London, Uingereza ambaye pia amewahi kuwa Balozi wa Uingereza nchini Belarus, amenukuliwa akisema Urusi imekutana na kikwazo kikubwa kutoka kwa Jeshi la Ukraine ambapo mpaka sasa, maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa Jeshi la Urusi, wakiwemo mabrigedia wawili wametekwa na wanajeshi wa Ukraine.

Naye Tom Bullock, mchambuzi wa taarifa za Kiintelijensia kutoka Kampuni ya Janes, amenukuliwa akisema mpaka sasa Urusi imeshindwa kutumia ukubwa wa jeshi lake na nguvu za kivita kulikamata Jiji la Kyiv ndani ya muda mfupi kama ilivyotarajiwa na wengi na kueleza kwamba hata katika miji mingine mbali na Kyiv, wanajeshi wa Ukraine wameendelea kufanya kazi kubwa ya kuwarudisha nyuma wanajeshi wa Urusi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!