Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari Poland yagoma kucheza na Urusi mchujo Kombe la Dunia
HabariMichezo

Poland yagoma kucheza na Urusi mchujo Kombe la Dunia

Spread the love

RAIS wa Chama cha Soka Poland, Cezary Kulesza amesema taifa hilo litakataa kuchuana na Urusi katika mechi ya mchujo ya kuwania Kombe la Dunia ili kupinga uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Mpinzani mwingine anayetarajiwa kucheza na Urusi ni Sweden ambaye pia wameunga mkono hatua hiyo.

“Hatuwezi kujifanya kuwa hakuna kinachoendelea,” alichapisha Robert Lewandowski kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Nyota huyo wa Bayern Munich alikuwa mmoja wa wachezaji wengi wa Poland waliounga mkono mara moja uamuzi wa Chama cha Soka Poland kugomea mechi ijayo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Urusi.

Haya ni maamuzi ya hivi punde kutoka kwa ulimwengu wa kandanda dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, huku vilabu vikiwa vimesitisha udhamini na makampuni ya Urusi.

Awali shirikisho la kandanda UEFA waliipokonya Urusi uwenyeji wa fainali ya ligi ya Mabingwa kutoka uwanja wa Saint Petersburg.

Hata hivyo, bado hakuna taarifa yoyote kutoka kwa waangalizi wa kimataifa wa FIFA kupiga marufuku Urusi kushiriki katika Kombe la Dunia, au UEFA kuvifukuza vilabu vya Urusi kutoka kwa mashindano yake.

Chama cha soka cha Poland wamechukulia hatua suala hilo mikononi mwao, huku rais wa shirikisho hilo Cezary Kulesza akiandika kwenye Twitter, “Hakuna maneno zaidi, ni muda wa vitendo!,”

Mataifa hayo mawili yalitarajiwa kumenyana mjini Moscow mwezi ujao, huku mshindi akicheza na Sweden au Jamhuri ya Czech kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia huko Qatar.

Sweden baadaye iliunga mkono msimamo wa Poland. “Timu ya kitaifa ya wanaume haitacheza dhidi ya Urusi, bila kujali ni wapi mechi itachezwa,” shirikisho la soka la Sweden lilichapisha kwenye Twitter.

Rais wa Poland, Andrzej Duda na Wwaziri mkuu, Mateusz Morawiecki pia walionyesha kuunga mkono hatua hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!