August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walimu wanawake walilia ndoa zao

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu

Spread the love

WALIMU wanawake wamelalamikia hatua ya serikali kuwapangia kazi katika vituo vya mbali kwa kuwa kunahataraisha ndoa na waume zao, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa mwalimu Joyce Kaishozi ambaye ni mwakilishi kitengo cha walimu wanawake katika manispaa ya Dodoma, wakati akisoma risala mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mdeme.

Mwalimu Kaishozi alisema walimu wanawake wanafanya kazi kubwa ya kuelimisha jamii, lakini wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa ambazo zinawafanya kufanya kazi bila kuwa na utulivu wa kiakili.

Amesema baadhi ya changamoto wanazokutana nazo ni walimu wanawake kuhamishwa vituo vya kazi na kupelekea mbali na hivyo kutengana na familia zao.

error: Content is protected !!