August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Huyu ndiye Lissu, alianza kupinga dhuluma akiwa mdogo

Spread the love

MDOGO wake, mwanasiasa machachari, Tundu Lissu, Vincent Lissu amefunguka na kueleza maisha ya kaka yake tangu akiwa anasoma shule ya msingi,  huku akisema ndugu yake alianza harakati za kupinga  ufisadi na kuonewa tangu miaka miaka ya 80.

Lissu ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa sasa ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema).

Vincent akizungumza na MwanaHALISI online, amesema ndugu yake Lissu ana msimamo usioyumba tangu akiwa mdogo na kwamba ameendelea kuishi hivyo mpaka leo.

“Kaka yangu amekuwa mtetezi wa haki tangu akiwa mdogo sana na hakupenda kuona uonevu mbele ya macho yake,” ndivyo anavyosema Vincent.

HAYA NI MAELEZO YA VICENT KUHUSU KAKA YAKE LISSU PAMOJA NA KUTOA HISTORIA YAKE, USISAHAU KU-SUBSCRIBE CHANNEL YETU YA YOUTUBE (MwanaHALISI TV)

error: Content is protected !!