August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakulima waiomba serikali mashamba ya kulima

Dk. Steven Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro

Spread the love

SERIKALI kupitia wizara ya kilimo na mifugo imeombwa kuangalia uwezekano wa kuwapatia mashamba wakulima wanaotoa elimu kwenye maonesho ya wakulima ya imo nane nane Kanda ya Mashariki, anaandika Christina Haule.

Ombi hilo limetolewa na wakulima mbalimbali katika Manispaa ya Kigamboni mbele ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe.

Mkulima kutoka banda la Kigamboni, Bakari Ndilana amesema wao kama wakulima wanaoonesha bidhaa za kilimo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi.

Ndilana amesema wakulima katika kikundi cha asilia kutoka Kigamboni jijini Dar es salaam hununua bidhaa mbalimbali na kutengeneza majani ya chai yanayosaidia kutoa sumu mwilini.

error: Content is protected !!