Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Walimu 29,879 waajiriwa miaka 2 ya Rais Samia
Elimu

Walimu 29,879 waajiriwa miaka 2 ya Rais Samia

Innocent Bashungwa
Spread the love

 

WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema tangu Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, Serikali imeajiri jumla ya walimu 29,879 wa Shule za Msingi na Sekondari.

Amesema takwimu zinathibishisha mkuu huyo wa nchi anathamini kada ya walimu. Anaripoti Danson Kaijage, Kagera … (endelea).

Hata hivyo, amesisitiza Serikali itaendelea kuboresha maslahi ya walimu nchini na imedhamiria kutatua na kumaliza kero za walimu nchini ikiwa ni pamoja na madaraja na stahiki zao mbalimbali.)

Amesema hayo tarehe 27 Oktoba 2023 wilayani Karagwe mkoani Kagera katika Sherehe ya kuadhimisha kilele cha siku ya Mwalimu Duniani na miaka 30 ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) yenye kauli mbiu “Walimu Tuwatakao kwa Elimu Tuitakayo, Lazima Kutatua Uhaba wa Walimu”

Bashungwa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan ambapo tangu aingie halmashauri ya wilaya Karagwe imeshapokea Sh 3.1 bilioni kuboresha elimu ya msingi na Sh 5.5 bilioni kuboresha elimu ya sekondari.

Kuhusu kanuni ya malipo ya mkupuo na malipo ya pensheni kwa wastaafu (Kikokotoo), amesema Serikali ya imeendelea kuwa sikivu na kuwathamini walimu wastaafu, na watumishi wote waliotumikiaa Taifa hili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuTangulizi

Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro

Spread the loveMwalimu Maganga Japhet amesimamishwa kazi na Tume ya Utumishi wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi...

error: Content is protected !!