MAMLAKA ya Mapato Tanzania imetoa wito kwa Watanzania kujiepusha na matumizi ya risiti na stempu feki ambazo zinaikosesha serikali mapato. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Hatua hiyo imekuja baada ya uwepo wa risiti na stempu feki ambazo nyingine hutengenezwa kutoka nje ya nchi na kuingizwa nchini kwa njia za magendo.

Akiwasilisha mada katika Mkutano Mkuu wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam(DCPC) jana Ijumaa, Msimamizi wa masuala ya Kodi, Lucas Igembe alisema hiyo ni changamoto kubwa inayoisumbua mamlaka hiyo.
Alisema ni vema wananchi kushirikiana na mamlaka hiyo kufichua wafanyabiashara hao wasio waaminifu ili kutokomeza tabia hiyo ambayo ni sawa na utengenezaji wa fedha feki.
Aidha, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo alisema kutokana na kukithiri kwa matumizi hayo ya stempu feku kutoka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu, wananachi wanaweza kuhakiki stempu za bidhaa wanazonunua kuwa kupakua programu ‘Hakiki App’ inayopatikana kwenye simu rununu.
“ Pia wanaweza kupiga pichi risiti ambazo wanahisi ni feki na kuituma kwenye kitengo maalumu cha TRA kupitia namba 0744233333 kwa njia ya mtandao wa Whatsap,” alisema.
Leave a comment