Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wadukuzi Korea Kaskazini waiba dola milioni 615 mtandaoni
Kimataifa

Wadukuzi Korea Kaskazini waiba dola milioni 615 mtandaoni

Spread the love

 

MAREKANI imewahusisha wadukuzi wanaoungwa mkono na Korea Kaskazini, na wizi mkubwa wa fedha za mtandaoni dola milioni 615 kutoka kwa wachezaji maarufu wa mchezo wa mtandaoni wa Axie Infinity Machi 2022. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa mashirika ya kimataifa … (endelea)

Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani wanasema, waliohusika na uhalifu huo ni kundi linaloitwa Lazarus Group linaloaminika kudhibitiwa na Ofisi Kuu ya Korea Kaskazini.

Udukuzi huo unaweza kuwa mojawapo ya matukio makubwa zaidi, ambayo hayakuwahi kutokea katika ulimwengu wa fedha za mitandaoni.

“Wanasema kupitia uchunguzi waliweza kuthibitisha kuwa Lazarus Group na APT38, watendaji wa mtandao wanaohusishwa na (Korea Kaskazini), wanahusika na wizi huo.”

Hata hivyo FBI katika taarifa yake iliyoitoa jana Alhamisi tarehe 14 Aprili 2022 ilieleza kundi la Lazarus lilipata sifa mbaya mwaka 2014, baada ya kushutumiwa kwa kuvamia picha za Sony na kuvujisha data za siri hadharani.

Aidha jopo la Umoja wa Mataifa linalofuatilia vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, limeishutumu Pyongyang kwa kutumia fedha zilizoibiwa kusaidia mipango ya nyukilia na makombora ya balestiki kama njia ya kuepuka vikwazo vya kimataifa.

Marekani inafahamu DPRK imezidi kutegemea shughuli haramu, ikiwa ni pamoja na uhalifu wa mtandao kuzalisha mapato kwa silaha za maangamizi na programu za makombora ya balestiki wakati inajaribu kukwepa vikwazo vikali vya Marekani na Umoja wa Mataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!