Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wataja tamu, chungu utekelezaji maendeleo endelevu
Habari Mchanganyiko

Wadau wataja tamu, chungu utekelezaji maendeleo endelevu

Spread the love

 

WAKATI Serikali ya Tanzania ikiongeza juhudi katika utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDG’s), ombwe la umasikini kati ya wananchi wa mijini na vijijini, limetajwa kukwamisha jitihada hizo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 14 Septemba 2023 na Muungano wa Asasi za Kiraia Zinazopambana na Umasikini Tanzania (GCAP Tanzania Coalition), wakati ukitoa tathimini yake juu ya mafanikio na changamoto zilizopatikana katika utekelezaji wa nusu muhula wa SDG’s, unaotarajiwa kufika tamati 2030.

Akizungumza wakati anatoa tathimini hiyo, Mratibu wa GCAP, Martina Kabisana, amesema umaskini umeendelea kuongezeka katika maeneo ya vijijini, kutokana na mamlaka kutoweka usawa katika ugawaji rasilimali fedha, pamoja na kufikisha miradi ya maendeleo.

“Licha ya hatua za maendeleo tulizopiga, umasikini umeendelea kuongezeka kwa kasi hasa kwa pengo kati ya watu wa vijijini na mijini kiuchumi kuongezeka, kukosekana kwa usawa wa kipato na ukosefu wa usawa wa huduma za jamii hasa vijijini na mijini bado changamoto,” amesema Kabisama.

Ametaja changamoto nyingine zilizoibuka katika utekelezaji wa SDG’s, ikiwemo kusuasua kwa utawala bora, uwazi na uwajibikaji na uharibifu wa mazingira.

“Tunashauri Serikali na wadau waongeze juhudi kupunguza pengo la umaskini mijini na vijijini na kuhakikisha kuwa hakuna atakayeachwa nyuma. Kuimarisha utawala bora, uwazi na uwajibikaji katika ngazi zote ili kuhakikisha ugawaji wa rasilimali za umma na utoaji huduma unakuwa wa ufanisi na usawa,” amesema Kabisana.

Alisema kutokana na changamoto hizo, GCAP itatumia wiki ya hamasa ulimwenguni juu ya utekelezaji malengo hayo 17, yaliyowekwa kwa ajili ya kuondoa umasikini.

Katika hatua nyingine, Kabisama ametaja mafanikio yaliyopatikana kwenye utekelezaji wa SDG’s, ikiwa pamoja na ongezeko la uandikishaji wanafunzi katika shule za msingi na sekondari, lililotokana na uamuzi wa Serikali kutoa elimu bure.

Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa kasi ya ukuaji uchumi na kupeleka Tanzania kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati 2019 na kuimarika kwa usawa wa kijinsia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

error: Content is protected !!