Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Vikosi vya Israel vyawaua Wapalestina 2
Kimataifa

Vikosi vya Israel vyawaua Wapalestina 2

Spread the love

 

WAPALESTINA wawili wauawa na vikosi vya Israel kwenye matukio tofauti huko Palestina. Anaripoti Glory Massamu TUDARCo kwa msaada wa mitandao ya kimataifa … (endelea)

Mauaji hayo yametokea leo Alhamisi tarehe 30 Septemba 2021, ambapo mtu mmoja ametambuliwa kwa jina la Alaa Nasser Mohammed Zayyoud, mwenye umri wa miaka 22, kutoka katika kijiji cha Burqin na mwanamke mmoja kutokea Jerusalem.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo, Zayyoud alipigwa risasi usiku katika kijiji cha burqin wakati akikabiliana kwa kutumia silaha na jeshi la Israel.

Israel ilivamia mji huo kwa kutumia gari kadhaa aina ya Jeeps za kijeshi na vikosi maalum alfajiri ya leo na kufanya shambulizi.

Wizara ya Afya ya Palestina imesema, Zayyoud alipigwa risasi nne, ambapo mbili za kifua, moja ya shingo na nyingine kwenye paja la kulia.

Mashuhuda wa tukio hilo wameviambia vyombo vya habari vya ndani kwamba sniper wa Israeli alimpiga risasi kwa karibu.

“Jeeps na jeshi likamzunguka, walizuia gari la wagonjwa kumfikia, baadaye wakaruhusu gari hilo kuja baada ya kuhakikisha kuwa amekufa,” ameyasema hayo shahidi wa tukio hilo.

Mpalestina wa pili kuuawa na majeshi ya Israel, ametambuliwa kama Israa Khuzaima mwenye umri wa miaka 30, mama wa watoto watatu, kutoka kijiji cha Qabatiya huko Jenin.

Hata hivyo, vikosi vya Israeli vimetangaza vilimpiga risasi Khuzaima kwa madai ya kwamba alijaribu kumchoma moto afisa mmoja.

Aidha, wakati operesheni za kijeshi za Israeli zikiendelea katika miji na vijiji, mashambulizi yamekua mengi kwa wakazi wa Palestina katika miezi michache iliyopita.

Agosti 2021, jeshi la Israel liliwaua Wapalestina wanne katika kambi ya wakimbizi ya Jenin wakati wa uvamizi uliosababishwa na makabiliano ya silaha.

Ambapo Jumapili tarehe 26 Septemba 2021, majeshi ya Israel yaliwaua wapalestina watano wakati wa makabiliano ya silaha kufuatia mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa huko Jenin na Jerusalem.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!